SIGARA ZA MENTHOL ZINA MADHARA MAKUBWA YA KIAFYA UKILINGANISHA NA SIGARA ZINGINE



Mamlaka ya chakula na dawa inchini marekani imesema sigara za menthol zina madhara ya kiafya zaidi ukilinganisha na Sigara nyingine.

Mamlaka hiyo imesema kwamba kutokana na tafiti zilizofanyika hivi karibuni zinaonesha kwamba Sigara za menthol zina mfanya mvutaji awe addicted kwa kuongeza kasi ya uvutaji na kushindwa kuziacha kwa urahisi hali anayosababisha mvutaji kuwa hatarini zaidi kupata Saratani na magonjwa mengine yanayosababishwa na tumbaku.

Pia mamlaka hiyo iliongeza kuwa Sigara za menthol ni chaguo la kwanza kwa asilimia 40 ya vijana wote wavutaji kwa kuwa zina radha ya menthol na hivyo huongeza hali ya hatari kwa group kubwa la watu.

No comments:

Post a Comment