UTAFITI: MAGONJWA YA SARATANI YANA UHUSIANO NA FAMILIA TUNAZOTOKA


Kuwa na Saratani kwenye familia kunaongeza uwezekano wa kuendelea kuwepo kwa saratani zaidi ya aina moja ndani ya Familia.

Utafiti uliofanywa huko Italia na Switzerland kwa watu 23,000 umegundua kwamba kwa kila Saratani kati ya Saratani 13 ambayo ndugu wa karibu aliwahi kuwa nayo huongeza uwezekano wa kutokea saratani inayofanana katika familia, lakini pia utafiti huo umepata uthibitisho kwamba historia ya familia iliyokuwa na aina moja ya saratani inaweza kuleta uwezekano wa kuibuka kwa saratani zingine.

Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida la ‘Annals of Oncology’ uliwafuatilia wagonjwa 12,000 wa saratani za aina tofauti na kuwalinganisha na watu 11,000 waliokuwa hawana Saratani.

Watafiti walikusanya taarifa za historia ya Saratani kwenye familia zao kwa kuwahusisha wale ndugu wa damu (first-degree relative) ambao wanachangia asilimia 50 ya genes mfano wazazi, watoto na wajukuu.

Watafiti waligundua kwamba watu ambao wana ndugu wa damu waliokuwa wakiugua Saratani ya njia ya hewa (larynx), walikuwa hatarini mara tatu kupata Saratani ya Kinywa (Oral) na pharyngeal.

Wale wenye ndugu wa damu ambao walikuwa wakiugua Saratani ya Kinywa na Pharyngeal walikuwa hatarini mara nne kupata saratani ya Oesophangeal, na wale wenye ndugu wa damu waliokuwa na Saratani ya Titi (breast Cancer) walikuwa hatarini mara mbili kupata Saratani ya mayai ya uzazi (ovarian cancer) kwa wanawake, na wanaume walikuwa hatarini mara 3.4 kupata Saratani ya Prostate kama ndugu wa damu alikuwa anaugua saratani ya kibofu (bladder cancer).

Pia utafiti uligundua kwamba ndugu wa kike wapo hatarini kupata saratani ya Titi (breast cancer) kama historia ya familia inaonesha kuliwahi kuwa na ndugu wa damu mwenye Saratani ya utumbo (bowel Cancer).

Kiongozi wa Utafiti huo Dr. Eva Negri kutoka Taasisi ya Mario Negri inayojihusisha na tafiti za madawa huko Milani alisema uhusiano huo wa Saratani unaweza kuongezeka kwenye familia iwapo kutakuwa na uhusiano mkubwa wa staili ya maisha ndani ya familia hiyo, mfano: uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe na sababu zingine za kimazingira zinazofanana.

Jessica Harris kutoka Taasisi ya utafiti ya Saratani ya UK alisema, hatari ya kupata Saratani (Cancer risks) hutegemeana na ufanano wa genes tunazorisi (inherit) kutoka kwa wazazi, staili za maisha tunazoishi na mazingira yetu.



Source: BBC Newz




No comments:

Post a Comment