Timu ya watafiti wa
chuo kikuu cha Cambridge wamegundua jinsi kinga ya mwili inavyochochewa na aleji ya paka na kusababisha matatizo kama
vile kukohoa na kupiga chafya, kutokana na utafiti huo kumeibuka na matumaini
mapya ya kuanzishwa kwa kinga mpya itakayozuia aleji hiyo.
Watafiti hao wakiongozwa
na Dr Clare Bryant wa chuo kikuu cha Cambridge waliifanyia utafiti protini
iitwayo DANDER inayopatikana kwenye ngozi ya Paka ambayo waliielezea ndiyo
inayosababisha aleji. Wamegundua kwamba aleji ya Paka huwa ina chochea
vichocheo vyamwili pale ambapo mwili huwa na kiasi Fulani cha sumu
zinazosababishwa na bacteria na hivyo kuufanya mwitikio wa kinga ya mwili kuwa
mkubwa kiasi cha kusababisha dalili mbaya kama vile kukohoa, kupiga chafya,
kuongezeka kwa mapigo ya moyo, na kupatwa na mafua.
Dr. Bryant aliliambia
shirika la habari la BBC “tumegundua jinsi ambavyo protini ya aleji ya Paka inavyochochea
chembechembe za kinga (immune cell) ya mtu, na kutokana na ugunduzi huo
tumetengeneza Dawa ambayo bado ipo kwenye majaribio (clinical trials) ya
magonjwa mengine kama vile sepsis (uwepo wa bacteria wanaodhuru au sumu zao
ndani ya mwili), na hivyo iwapo itaonesha mafanikio mazuri basi inaweza
kutumika kama tiba na kinga dhidi ya aleji ya Paka.
Bofya HAPA kusoma zaidi
No comments:
Post a Comment