Arsenic ni elementi ya sumu inayopatikana ardhini na
majini ikiungana sulfa au metali zingine.
Kwa muda mrefu Arsenic imekuwa ikijulikana kusababisha
madhara kwa binadamu, madhara hayo ni saratani, magonjwa ya moyo, na magonjwa
ya ufahamu. Utafiti mpya wa hivi karibuni umebaini kwamba kunywa maji yenye
kiasi kidogo sana cha elementi ya Arsenic kunaweza kuharibu mapafu, na kuongeza
kwamba madhara yanaweza kuwa makubwa zaidi iwapo itaingia kwa mtu anaevuta
sigara.
Utafiti huo ulikuwa ni sehemu ya mradi wa muda mrefu
ambao ulifanywa Bangladesh inchini India, ambapo takribani nusu ya watu wapatao
milioni 77 wanaishi kwenye maeneo yenye visima vya maji (groundwater wells)
vilivyosheheni kiwango kikubwa cha elementi za arsenic.
Kwa muda wa zaidi ya miaka mitano, watafiti walikuwa
wakijaribu kupima uwezo wa mapafu kwa wagonjwa 950 ambao walihudhuria kwenye
vituo vya afya kwa matatizo ya mfumo wa hewa (upumuaji). Vipimo vya wagonjwa
hao vililinganishwa na kiasi cha arsenic kilichokutwa ndani ya miili yao. Matokeo
yalionyesha kwamba athari za arsenic kwenye mapafu zinatofautiana kulingana na
kiasi cha arsenic (Dose) kilichoingia kwa mgonjwa, matokeo hayo yalichapishwa kwenye jarida la America Journal of Respiratory and Critical Care Medicine.
Watu waliokunywa maji yenye kiwango nusu ya kile
kinachokubaliwa kimataifa hawakuonyesha dalili zozote za madhara ya mapafu,
wale waliokunywa maji yenye kiasi cha arsenic mara 10 ya kile kilichoruhusiwa
walionyesha dalili za kushindwa kupumua vyema (Loss of breathing function),
wale waliokunywa maji yenye arsenic zaidi ya mara kumi (10>) ya kiwango
kilichoruhusiwa walionyesha dalili mbaya zaidi za kushindwa kupumua sawasawa na
mtu aliyevuta tumbaku kwa miongo (decades) mingi na kuwafanya wawe hatarini kupata
magonjwa hatari ya njia ya hewa (serious respiratory diseases).
Kujua kiwango cha arsenic kilichoruhusiwa kwenye maji
ya kunywa Tanzania BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment