UTAFITI: MAJI SAFI NA SABUNI ‘HUSAIDIA UKUAJI’ KWA WATOTO



Upatikanaji wa maji safi na sabuni sio tu unaboresha usafi lakini pia unaweza kuchochea (boost) ukuaji kwa watoto wadogo, imeshauriwa na Utafiti.

Wafuatiliaji wa takwimu za tafiti zilizofanyika ulimwenguni wamepata uthibitho kwamba watoto chini ya umri wa miaka mitano wanaoishi kwenye kaya zenye mazingira bora ya usafi (good sanitation) huongezeka kimo cha sentimita 0.5 ukilinganisha na wanaoishi kwenye mazingira machafu.

Ufuatiliaji wa takwimu hizo ulifanyika katika nchi za Bangladesh, Ethiopia, Nigeria, Chile, Guatemala, Pakistan, Nepal, South Africa, Kenya na Cambodia.

Kwa mujibu wa takwimu za WHO, ukuaji hafifu huwakumba watoto takribani milioni 265 ulimwenguni kote na kuwaacha wakiwa na madhara lukuki ya kiafya.

Akiongea na shirika la habari la BBC, kiongozi wa wafuatiliaji wa takwimu hizo, Dk. Alan Dangour kutoka London School of Hygiene & Tropical Medicine (LSHTM) amesema kwamba kuwapatia watoto maji safi, usafi wa mazingira (sanitation) na usafi wao (hygiene) ni jambo bora litakalopunguza vifo vinavyotokana na dalili za magonjwa kama vile kuharisha.

Uchambuzi umeonesha kwamba iwapo mtoto atazipata huduma hizi akiwa bado mdogo anaweza kupata jambo dogo lakini ni muhimu sana nalo ni ukuaji bora, alisema Dk.Dangour

Amesema kwamba kuna uhusiano ulio wazi kati ya watoto kunywa maji machafu, kupata magonjwa ya kuhara na hivyo kupata ukuaji dhaifu (kudumaa), kwasababu majonjwa yanayojirudiarudia kipindi cha utotoni yanaathiri ukuaji.



Kusoma zaidi BOFYA HAPA



No comments:

Post a Comment